MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHARLES MAULA (55) MKAZI WA NKUNG’UNGU WILAYA
YA CHUNYA ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA SHOKA KICHWANI NA KISHA MWILI
WAKE KUTUPWA PORINI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA PORINI MNAMO TAREHE 11.10.2014 MAJIRA YA SAA 18:00
JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LWIKA, KIJIJI CHA NKUNG’UNGU, KATA YA
LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI YA KUKATWA KWA SHOKA.
CHANZO
CHA MAUAJI HAYO INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA ANADAIWA TSHS. 300,000/=.
WATUHUMIWA WATATU WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1.
MASANILO MBOJE (59) 2. MASHALA MASANILO (30) NA 3. MACHIA MAGALAGO (31)
WOTE WAKAZI WA LWIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
BWENI
MOJA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MBALIZI LIITWALO “NKURUMAH WINGI C”
LIMEUNGUA MOTO NA KUSABABISHA HASARA NA UHARIBIFU WA MALI ZOTE
ZILIZOKUWEMO NDANI YA BWENI HILO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.10.2014 MAJIRA YA SAA 20:45 USIKU HUKO
MBALIZI, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI, MKOA WA MBEYA. MWANAFUNZI MMOJA WA KIDATO CHA TATU KATIKA
SHULE HIYO ALIFAHAMIKA KWA JINA LA KILIAN MOSHI @ MSYANI (15) ALIGUNDUA
KUUNGUA KWA BWENI HILO. MOTO HUO ULITEKETEZA VITANDA NANE NA MAGODORO NA
MALI ZOTE ZILIZOKUWEMO NDANI YA BWENI HILO NA KUSABABISHA UHARIBIFU NA
HASARA KUBWA.
CHANZO
CHA MOTO HUO BADO HAKIJAFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA
KUTOKANA NA MOTO HUO PIA BADO KUFAHAMIKA. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU
YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. AIDHA, MOTO HUO ULIZIMWA KWA JITIHADA ZA KIKOSI
CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, ASKARI POLISI NA WANANCHI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA MATUKIO
YATOKANAYO NA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO
KATIKA MAJENGO YAO ILI KUWEZA KUKABILIANA NA MAJANGA KAMA HAYO PINDI
YANAPOTOKEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KIGAMBONI WILAYA
YA CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IGNAS ISACK JOHN (30) AKIWA NA POMBE
YA MOSHI UJAZO WA LITA 011/2.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA KIGAMBONI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA
KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA
MTUMIAJI WA POMBE HIYO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment