TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHARLES MAULA (55) MKAZI WA NKUNG’UNGU WILAYA YA CHUNYA ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA SHOKA KICHWANI NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA PORINI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA PORINI MNAMO TAREHE 11.10.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LWIKA, KIJIJI CHA NKUNG’UNGU, KATA YA LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI YA KUKATWA KWA SHOKA.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA ANADAIWA TSHS. 300,000/=. WATUHUMIWA WATATU WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. MASANILO MBOJE (59) 2. MASHALA MASANILO (30) NA 3. MACHIA MAGALAGO (31) WOTE WAKAZI WA LWIKA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
BWENI MOJA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MBALIZI LIITWALO “NKURUMAH WINGI C” LIMEUNGUA MOTO NA KUSABABISHA HASARA NA UHARIBIFU WA MALI ZOTE ZILIZOKUWEMO NDANI YA BWENI HILO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.10.2014 MAJIRA YA SAA 20:45 USIKU HUKO MBALIZI, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA. MWANAFUNZI MMOJA WA KIDATO CHA TATU KATIKA SHULE HIYO ALIFAHAMIKA KWA JINA LA KILIAN MOSHI @ MSYANI (15) ALIGUNDUA KUUNGUA KWA BWENI HILO. MOTO HUO ULITEKETEZA VITANDA NANE NA MAGODORO NA MALI ZOTE ZILIZOKUWEMO NDANI YA BWENI HILO NA KUSABABISHA UHARIBIFU NA HASARA KUBWA.
CHANZO CHA MOTO HUO BADO HAKIJAFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA KUTOKANA NA MOTO HUO PIA BADO KUFAHAMIKA. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. AIDHA, MOTO HUO ULIZIMWA KWA JITIHADA ZA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, ASKARI POLISI NA WANANCHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA MATUKIO YATOKANAYO NA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO KATIKA MAJENGO YAO ILI KUWEZA KUKABILIANA NA MAJANGA KAMA HAYO PINDI YANAPOTOKEA.

TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KIGAMBONI WILAYA YA CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IGNAS ISACK JOHN (30) AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 011/2.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIGAMBONI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Post a Comment

أحدث أقدم