Msanii wa muziki wa taarab na mduara, Hammer Q yupo mbioni
kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Jero’ ambapo pia ametoa sababu ya
kushindwa kutoa video ya Kibakuli kama alivyowahidi mashabiki wake.
“Wengi walitegemea video ya Kibakuli lakini nikaona kuna mahitaji
makubwa sana kwenye muziki wangu, watu wanahitaji muziki wangu. Kwahiyo
nikaona huku wadau wakiendelea kusubiri video ya Kibakuli wapokee kazi
yangu mpya inayokwenda kwa jina Jero. Video nimefanya na kampuni inaitwa
Paradise video iliyoko Arusha, naomba wadau wanisupport,”.
Post a Comment