HAWA NDIO MAJERUHI WA AJALI YA LORI LA MAFUTA LILILOWAKA MOTO MBAGALA USIKU WA KUAMKIA LEO



Watu watatu wamefariki na wengine sita  wakiwa katika hali mbaya Hospitali ya Muhimbili kufuatia tukio la moto uliolipuka kwenye gari la kubeba mafuta  jana maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
 
Alizumgumza na mwandishi, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohammed Mpinga, alisema ajali hiyo haikuleta athari yoyote baada ya gari lile kupata ajali ila athari ilijitokeza baada ya watu kuvamia na kuanza kuiba mafuta na baadaye kujaribu kuiba betri ndipo cheche za moto zilipolipuka na kusababisha kuwaka kwa gari hilo.
 
Wakati huohuo,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam Mecky Sadick, amewataka wananchi kutokuwa na tabia ya kuvamia ama kuiba vitu pindi ajali zitokeapo.
 
Sadick alisema hayo alipotembelea hospitali ya Muhimbili na Temeke walipolazwa majeruhi hao.
picha na gpl

Post a Comment

أحدث أقدم