Ni
kawaida kusikia mtu kapewa ‘a.k.a’ ambayo lazima kuna kitu
kilichopelekea akapewa a.k.a hiyo, huenda ikawa ni muonekano wake,
tabia, mavazi ama kitu chochote kile kinachohusiana na yeye.
Watu wamekuwa wakitoa ‘a.k.a’ hata kwa vitu vingine pia, lakini kali
ni hii kutoka Marekani, ambapo ripota wa kituo cha televisheni cha CNN
alitoka kali baada ya kutoa a.k.a ya ugonjwa wa Ebola, kwa kuuita
“Fear-bola”
Mel
Robbins amenukuliwa katika ukurasa wa mtandaoni wa kituo hicho akisema;
“Fear-bola inashambulia sehemu ya ubongo inayohusika na kuwaza mambo ya
busara”
Mtangazaji huyo aliongezea kuwa ‘Fear-bola’ ilianza pale
ilipogundulika wauguzi 2 walipata maambukizi hayo huko Dallas, na
baadaye ikatanda ‘ugonjwa wa hofu’ kila kona ya Marekani.
إرسال تعليق