Ripoti kutoka Vatican inasema ’Kanisa inabidi iwaruhusu na kuwakaribisha wapenzi ambao wapo kwenye mahusiano ya jinsia moja’.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika Oct 13
ambao ulifanyika Jumatatu ili kutoa ripoti hiyo, Kadinali ‘Luis Antonio
Tagle wa Philippines alisema ‘Wakatoliki wanafuatilia sana maswala ya
umaskini, vita na uhamiaji na kuacha swala la watu ambao wapo kwenye
mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja’.
Lugha hii mpya ya kuhusiana na mapenzi kati ya watu wa jinsia moja inalinganishwa na ‘utetemeko wa Mapasta’, alisema mmoja kati ya waandishi wa habari wa Vatican. ‘Swala la mahusiano ya wapenzi wa jinisia moja linaenda mbali sana mpaka kanisa nalo linajiuliza kama nalo likubali swala hilo bila kuharibu kanuni, sheria na imani za Kikatoliki’, alisema John Thavis.
Mchungaji James Martin ambae pia ni mwandishi wa neno la Mungu
aliiita ripoti hii ya kuhusiana na mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja
kuwa ni tendo la “kimapinduzi’, aliendelea kusema kuwa mabadiliko
yanayofanywa na kanisa la Kitatoliki kuhusu mahusiano ya wapenzi wa
jinsia moja ni mazuri.
Aliongezea na kusema, ‘watu ambao wapo kwenye mahusiano ya mapenzi ya
jinsia moja nao wana uwezo mkubwa wa kuchangia kwenye jamii yetu ya
Kikristo’.
Wakatoliki wanaviita vitendo vya mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja ‘vitendo visivyo na utaratibu’.
Papa Francis, wakati anaongelea swala la kanisa la Kikatoliki mwaka
2013 alisema ‘mimi ni nani mpaka niwahukumu watu ambao wapo kwenye
mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja?’.
Kwa ripoti iliyotolewa jana Oct 13 muhtasari wa wiki nzima kuhusiana
mkutano uliofanywa na karibu Askofu 200, Makardianali na Makuhani pamoja
na Papa Francis unaendelea, lakini mpaka sasa hamna mabadiliko yoyote
ambayo yamefanywa.Majadiliano yanaendelea wiki hii na ripoti ya mwisho
itatolewa mwisho wa wiki hii.
إرسال تعليق