Kamati
ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi TFF, imemfungia wakili Damas
Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya
kiasi cha pesa.
Ndumbaro
ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal
Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia
tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka
kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv.
Ndumbaro
alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu
zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo
litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya
sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani
wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na
rais wa Shirikisho, Malinzi.
Kikao
cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro
na kumlilipisha faini kwa sababu. Ndumbaro ambaye alizungumza kama
wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa ‘ hadharani’
na vilabu huku vikisema kuwa ‘ havikumtuma’ kuzungumza yale ambayo
alisema mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa ‘
utashi’ wake mwenyewe, na si wao walimtuma.
‘
Kilichomuhuku’ ni yeye kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji
ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana.
Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu.
Ndumbaro
amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya
klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini yeye alijizungumzia
tu kama vile alivyotaka iwe.
via>>shaffihdauda.com
Post a Comment