Hivi
karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth
Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye
kusisimua iitwayo “MAPENZI YA MUNGU”
ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha
ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo
Marehemu Steven Kanumba.
Filamu ya “Mapenzi ya Mungu”
ni moja ya filamu ambayo Lulu ameonyesha uwezo wa hali ya na
kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike hapa Tanzania ambae
ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa
kubadilika badilika kutokana na muongozo anaopewa.
Filamu ya “Mapenzi ya Mungu” itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.
Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.
Post a Comment