Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni kiongozi
wa ujumbe kutoka Tanzania na anawakilisha kama Gavana Mbadala (Alternate
Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni
Gavana katika mikutano hii. Katika picha viongozi hao wakiwa wanafanya
majumuisho ya majadiliano ya awali na kukubaliana cha kufanya kwa pamoja
na viongozi kutoka IMF na WB kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya
sera za fedha na sera za mapato na matumizi.
Bw.Herve’
Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya
Mashariki akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile hayupo katika picha,
alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na
IMF na WB.
Dr.
Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa
serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania.Wakichukua mapendekezo
kutoka kwa viongozi wa IMF na WB hawapo kwenye picha. Kutoka kushoto ni
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania akiwa amefuatana na Bi. Natujwa Mwamba
Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kulia ni Bw. Philip
Mpango Katibu Mtendaji tume ya Mipango akifuatiwa na Msaidizi wa
kamishna sera Bw. Shogholo Msangi na wa mwisho ni Kamishna wa Bajeti Bw.
John Cheyo na walioketi nyuma wote ni wajumbe kutoka Tanzania
إرسال تعليق