Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni akitowa Mada
katika Kongamalo la kuzungumzia Katiba Mpya ya Tanzania baada ya
kupitishwa na Bunge Maalum la Katiba lililom,alizia kazi hiyo wiki
iliopita, akisoma baadhi ya Vifungu vilivyopitishwa na Bunge hilo.
Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserekali ya Tanzania
Yuoth Icon (TAYI) lililowakutanisha Vijana mbalimbali katika ukumbi wa
Ekrotanali.
Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika Kongamano hilo la Vijana
kuzungumzia Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano iliopitishwa na Bunge
Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
Vijana wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Ekrotanali Zanzibar.
Kijana Mtaalam wa Lugha za Ishara katika Kongamano hilo akitowa ishara
ya mazungumzo kwa Vijana wenye ulemavu wa kutokusikia walioshiriki
katika Kongamano hilo katika ukumbi wa Ekrotanali.
Baadhi ya Vijana wanaoshiriki Kongamano la Vijana kuzungumzia Katiba
Mpya ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Mbunge wa
Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika Kongamano hilo
lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserekali ya TAYI na kuwakutanisha
Vijana mbalimbali kuzungumzia Katiba. Kutoa elimu ya kuifahamu Katiba
hiyo
Vijana wakichagia na kutaka kujuwa baadhi ya Vifungu vya Katiba kutoka
kwa Aliyekuwa Mbunge wa Bunge Maal;um la Katiba na Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni, alipokuwa akisoma baadhi ya vifungu
hivyo katika Kongamano hilo.
Vijana walikuwa na hamu ya kujuwa na kutaka ufafanuzi kwa baadhi ya
vifungu vya Katiba ilioyopendekezwa na Wabunge wa Bunge Maalum la
Katiba, lililomaliza kazi hiyo wiki iliopita mjini dodoma.
إرسال تعليق