Mchezaji
wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na
majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao
lake.
Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti
wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la
kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari
West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa
kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema :
''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha
mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa
soka na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''
Post a Comment