Msanii
Emmanuel Simwinga maarufu Izzo Business akipiga bonge la shoo kwenye
Tamasha la Tigo Welcome Pack uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma. Kifurushi
cha welcome pack kinatoa muda wa maongezi wa dakika 20, MB175, sms bila
kikomo na shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo
kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.
Wasanii
wa Original Komedi wakiwapa burudani wananchi waliojitokeza kwenye
uzinduzi wa welcome pack kwenye uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma mwishoni
mwa wiki. Ziara ya Tigo welcome pack itaendelea mkoani Arusha Jumapili
ya wiki hii.
Mratibu
wa Masoko wa Tigo kanda ya Kaskazini na Kati Bw.Saitoti Naikara
akiongea na umati uliojitokeza kwenye uzinduzi wa welcome pack uwanja wa
Jamhuri Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Wateja
wakipata maelezo toka kwa watoa huduma wa kampuni ya Tigo ndani ya basi
la Kidigitali lililokuwepo uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma mwishoni mwa
wiki, wakati wa ziara ya Tigo ya kampeni ya welcome pack mkoani humo.
Post a Comment