Kunea kwa ugonjwa wa Ebola umefanya fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kuwa mashakani.
Fainali
hizo zimepangwa kufanyika nchini Moroco kuanzia Januari 17 lakini nchi
hiyo iliwaeleza waandaji wa mashindano hayo kwamba wangependa kusogeza
mbele mashandano hayo.Serikali ya Moroco imekuwa na wasi wasi maambukizo ya virusi vya ebola kutoka nchi za magharibi mwa Afrika.
Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF linatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho mwezi novemba kama nitasogeza mbele mashindano hayo au la japo limekuwa likisisitiza kuwa mashindano hayo yatafanyika kama kawaida
Wakati huo huo kumekuwa na taarifa kuwa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limeizungumzia nchi za Ghana na Afrika kusisni ili kama zinaweza kukubali kuwa fainali hizo.
Baada ya ligi mbalimbali duniani kusimama kwa muda ili kupisha mechi za timu za taifa, hekaheka za ligi hizo zinataraji kuendelea tena kesho.
Huko England nyasi za viwanja kadhaa zitakuwa matatani pale timu mbalimbali zitakaposhuka dimbani.
Katika uwanja wa Etihad wenyeji Manchester City watajitupa dimbani kuwakaribisha Tottenham katika mechi itakayotangazwa moja kwa moja na Idha ya Kiswahili ya BBC kuanzia saa saa nane na nusu kwa saa Afrika Mashiriki.
Mechi nyingine zitakazochezwa hiyo kesho ni kati ya Arsenal watakapowakaribisha Hull City, Burnley itapepetana West Ham, Crystal Palace watawakaribisha Chelsea, huku Everton watakuwa nyumbani kumenyana na Aston Villa.
Nayo Newcastle watavaana na Leicester City wakati Southampton itakuwa nyumbani kukwaana na Surnderland.
Siku ya Jumapili Liverpool watakuwa ugenini dhidi ya QPR nayo Stocke City watacheza dhidi ya Swansea City.
Nchini Tanzania kesho itakuwa ni siku ya wepenzi wa soka kwani watani wa jadi Simba na Yanga watakuwa katikauwanja wa Taifa uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
إرسال تعليق