Mkubwa Fella athibitisha YP kufariki dunia na Kusema Haya

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjA9SVLY73DLOp28RIC0DiBi-LpWm5zd_V71AXC7cyM5sR5g8GZh0X-taNEYFSXRvtR8ODvyQd3q8Wk4Xb16kNLUpOlzOcXLGQZg9tc3J_eW7Bbj9picCPcAMe4O-x0zndAdYE3zfBj0Y4/s400/YP.jpg
YP enzi za uhai wake

http://www.bongo5.com/wp-content/old/stories/fella_l.jpg
Said Fella
MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family aliye pia mkurugenzi wa MKubwa na Wanae, Said Fella 'Mkubwa' amethibitisha kuwa msanii YP amefariki dunia usiku wa kumakia leo.
Akizungumza hivi punde, Fella alisema YP amefariki akiwa katika Hospitali ya Temeke na siyo nyumbani kwao kama taarifa za awali zilizokuwa zimetufikia na kwamba alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kifua.
'Ni kweli YP amefariki akiwa Temeke Hospitali alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa, alikuwa akisumbuliwa na Kifua, kwa kweli ni pigo kwetu na tasnia nzima ya muziki kwani ni hivi karibuni tumetoka kumpoteza pia Side Mnyamwezi," alisema Fella mmoja wa wadu wa muziki waliosaidia kukuza muziki wa kizazi kipya kwa kuibua vipaji kila uchao. 
Fella alisema kwa sasa wanasubiri kuwasiliana na ndugu na familia ya marehemu YP kwa ajili ya kujua mazishi yake yatafanyika lini na wapi, japo alisema huenda akazikwa leo pande za TMK.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.

Post a Comment

أحدث أقدم