MKULIMA AKUTWA AMECHINJWA NA MWILI WAKE UKIWA UMEHARIBIKA MUHEZA TANGA

Watu wasiojulikana wamemvamia na kumchinja mkulima wa kijiji cha Mtindiro Wilayani Muheza, Richaridi Saidi, na kisha kumfungia katika nyumba yake.
 
Akizungumza nasi, Afisa Mtendaji wa kata ya Mtindiro, Ester Kaima, alisema kuwa mkulima huyo aliuawa na watu hao na kufungiwa ndani ya nyumba yake katika shamba la mmiliki wake Halidi Semboni.
 
Alisema baada ya watu kufanya mauaji hayo walitokomea kusikojulikana.
 
Alisema mwili wa mkulima huyo uligundulika siku ya tatu baadaye baada ya majirani kusikia harufu ikitoka ndani ya nyumba hiyo.
Katika tukio jingine Salima Rashidi amejiua kwa kunywa sumu.
 
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kwabada kata ya Mtindiro.
 
Jeshi la polisi wilayani Muheza limedhibitisha kutokea matukio hayo.
 
Na Steve William 

Post a Comment

Previous Post Next Post