Makundi
ya kikatoliki yanayopigania haki za wapenzi wa jinsia moja yameelezea
ghadhabu yao kutokana na hatua ya maaskofu wa kanisa hilo ya kukataa
mapendekezo ya kutangaza msimamo kuhusu mashoga, wasagaji pamoja na watu
waliotalakiana na wanaoana.
Wakati wa kumalizika kwa mkutano wa
maaskofu wa kanisa katoliki, Vatican ilishindwa kupata theluthi mbili ya
kura za maskofu wa kuunga mkono maoni yao kuhusu masuala hayo.
Kundi
la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Marekani la New Ways
Ministry limesema kuwa hatua ya maskofu hao kuamua kujadili suala hilo
ni matumaini ya siku za usoni.
Masuala hayo yanatarajiwa kuzungumziwa tena baada ya mwaka mmoja.
Post a Comment