Onyo la TCU kuhusu waliodahiliwa moja kwa moja Vyuo Vikuu


TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ina mamlaka kisheria kusimamia na kuratibu udahili wa Wanafunzi wote wanaojiunga na Vyuo Vikuu vyote nchini Tanzania.

Tume imebaini kuwa, hivi karibuni baadhi ya Vyuo Vikuu vimekuwa vikitangaza kudahili Wanafunzi moja kwa moja kupitia Vyuo vyao kwa mwaka wa masomo 2014/2015. Ifahamike kuwa, utaratibu unaotambulika kisheria ni wa kudahili Wanafunzi kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na si vinginevyo. Hivyo mwanafunzi atakayeomba na kupatiwa udahili kupitia Chuoni
moja kwa moja, udhili wake hautatambulika.

Tume inapenda kusisitiza kuwa waombaji wote wenye sifa za kujiunga na Vyuo Vikuu wanapaswa kufuata tartibu na miongozo iliyowekwa na Tume.

Taarifa hii imetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu.

Kwa mawasiliano zaidi, barua pepe es@tcu.go.tz na/au simu +255 222772657

Post a Comment

أحدث أقدم