SAFARI ALL AFRICA TOURNAMENT YAANZA LEO DAR

Mshiriki toka Kenya akionyesha ujuzi wake.
Mshiriki toka Afrika Kusini akionyesha ufundi huku washiriki toka Kenya wakimtazama. Mshiriki wa kike wa pool toka nchini Kenya akiwa kwenye mchezo huo. Mshiriki wa kike toka Tanzania. Wachezaji pool toka Zambia wakiwa katika pozi. Washiriki wa kiume toka Afrika Kusini wakijadiliana jambo. Washiriki wa pool wa kike toka Kenya. Washiriki wa timu ya Pool ya Tanzania wakiwa katika pozi. Muonekano wa meza kuu.
MASHINDANO ya pool yanayodhaminiwa na Safari Lager yameanza rasmi leo, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Budget ulioko Kunduchi.
Katika mashindano hayo yatakayomalizika tarehe 18 Oktoba yatahusisha timu za taifa za nchi zaidi ya 6 za  Afrika, Uganda, Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Cameroon na wenyeji Tanzania, zitachuana vikali  huku mshindi wa kwanza atajinyakulia zawadi ya dola 5oo, wa pili dola 300.

Post a Comment

أحدث أقدم