Wananchi
wenye ghazabu kali wamemshambulia kwa ngumi na mateke
kisha kumkamata askari wa usalama barabarani asiyefahamika
jina lake maeneo ya Ubungo - Dar es Salaam baada ya
kusababisha ajali.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, askari huyo alisababisha
ajali hiyo wakati akiongoza magari baada ya kuita magari
kutoka pande mbili kwa wakati mmoja, ambapo baada ya kuona
wamechoka muda mrefu kwenye foleni baadhi ya waendesha
magari hao walishuka kwenye gari zao na kumfuata kisha kuanza
kumshambulia ambapo jamaa mmoja alionekana kumpiga mtama
afande huyo na kumpaisha juu kimo cha ng'ombe kisha kudondoka
chini.
Hata
hivyo afande huyo aliona atoke nduki kwa ajili kuokoa mtima
wake lakini hakufika popote ambapo alikamatwa na kuendelea
kupigwa ngumi za chembe na kusababisha kushindwa kupumua
Pichani raia wakimlazimisha askari huyo kuingia kwenye bajaji ili kumfikisha kituo cha polisi.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ
إرسال تعليق