Meneja
Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam
(DAWASA) Bi. Neli Msuya alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
mwishoni mwa wiki walipotembelea mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati
endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) katika shule ya sekondari
Manzese iliyopo Mtaa wa Chakula bora kata ya Manzese Wilaya Kinondoni
jijini Dar es salaam. Mradi huo unatekelezwa shuleni hapo na DAWASA kwa
kushirikiana na Shirika la Mpango wa Makazi la Umoja wa Mataifa
(UN-HABITAT).
Na Eleteri Mangi- MAELEZO
Shule
ya sekondari Manzese itarajiwa kunufaika na mradi wa ujenzi wa mtambo
wa kuzalisha gesi ambayo ni nishati endelevu rafiki nainayohifadhi
mazingira nchini (Biogas).
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Majisafi na
Majitaka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari mwishoni mwa wiki walipotembelea mradi wa ujenzi wa
mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) katika shule
ya sekondari Manzese iliyopo Mtaa wa Chakula bora kata ya Manzese Wilaya
Kinondoni jijini Dar es salaam.
Bi.
Neli alisema kuwa mradi huo unatekelezwa shuleni hapo na DAWASA kwa
kushirikiana na Shirika la Mpango wa Makazi la Umoja wa Mataifa
(UN-HABITAT) ili kupata gesi ambayo pia itasaidia upatikanaji wa umeme
mbadala utakaotumika kwa matumizi mbalimbali na kuboresha taaluma kwa
wanafunzi.
Meneja
wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira
(Biogas) kutoka UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa akisisitiza jambo kwa
waandishi wa habari walipotembelea mradi huo unaotekelezwa katika shule
ya sekondari Manzese mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Baada
ya kutambua kuwa zaidi ya asilimia 80 ya majisafi yanayotumika hugeuka
kuwa maji taka, Bi. Neli amesema kuwa endapo kiasi hicho cha majitaka
kisipodhibitiwa ipasavyo neema hiyo ya kuongezeka kwa majisafi inaweza
isionekane.
“Shule
haitalazimika kufikiria majitaka hayo yaende wapi kwani DAWASA inatoa
suluhisho na imechukua jukumu la kuhakikisha maji hayo yanatumika
kuzalisha gesi ambayo ni rafiki kwa mazingira na afya za wanafunzi,
walimu na wanaozunguka maeneo ya shule” alisema Bi. Neli.
Bi.
Neli ameongeza kuwa sanjari na ujenzi wa mtambo huo wa gesi
unaoendelea, pia ujenzi wa maabara kwa masomo ya sayansi ambazo
zitatumia gesi itakanayotokana na majitaka yanayozalishwa shuleni hapo
unaendelea kwa ushirikiano na UN-HABITAT ili kuboresha taaluma.
Mratibu
wa Mradi ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi ambayo ni nishati endelevu
inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka Taasisi ya Kuendeleza Nishati
Asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) Shima Sago akieleza faida
zitokanazo na biogas kwa waandishi wa habari walipotembelea mradi huo
unaotekelezwa katika shule ya sekondari Manzese mwishoni mwa wiki jijini
Dar es salaam.
Kwa
upande wake Meneja wa Mradi huo nchini kutoka UN-HABITAT Phillemon
Mutashubirwa amesema kuwa gesi hiyo itatumika kwenye maabara ambazo
zinajengwa shuleni hapo kuitikia wito wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alioutoa kuwa shule zote ziwe
zimejenga maabara kwa masomo ya Kemia, Fizikia na Biyolojia ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu.
Naye
Mratibu wa Mradi wa kujenga mtambo wa kuzalisha gesi ambayo ni nishati
endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka Taasisi ya Kuendeleza
Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) Shima Sago amesema
kuwa kukamilika kwa mradi huo utakuwa na faida nyingi kwa shule na jamii
inayoizunguka shule hiyo.
Shima
amezitaja faida hizo kuwa ni pamoja na gesi hiyo itakuwa ya bei nafuu
ambapo gharama yake ni ya chini kutokana na malighafi kupatikana shuleni
hapo na nishati hiyo inajitosheleza kwa mazoezi ya wanafunzi maabara,
kupikia kwenye kantini ya shule, kuwasha taa kwa ajili ya wanafunzi
kujisomea pamoja na ulinzi na usalama wa shule.
Mwalimu
wa Taaluma wa shule ya sekondari Manzese Zubeda Kindamba akiushukuru
uongozi wa DAWASA kwa kuendelea kuiunga mkono shule yao katika masuala
mbalimbali ukiwemo Mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi asilia
shuleni hapo.
Shima
ametaja faida nyingine ni kutibu majitaka yanayotokana vyoo na kuondoa
athari ambazo ni chanzo cha magonjwa hatari kwa afya za wanafunzi na
jumuiya nzima inayoizunguka shule hiyo.
Aidha,
Shima amesema kuwa gesi itakayozalishwa katika mradi huo ni ujazo wa
kyubiki mita 200 ambazo zitakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kilowati
50 ambao utatosha kwa matumizi ya shule.
Vilevile
Shima amesema kuwa mradi huo utagharamu zaidi ya Sh. Milioni 70 za
Kitanzania ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka
huu tayari kuanza kutumika mwezi Januari 2015.
Kwa
upande wa wanafunzi, Noela Shirima mwanafunzi wa kidato cha nne
anayesoma masomo ya mchepuo wa sayansi amesema kuwa kujengwa mradi wa
gesi na maabara utawasaidia kufanya mazoezi mengi ameahidi kuwa
watatumia muda wao vizuri ili kuboresha taaluma yao ili waweze kufikia
malengo yao waliojiwekea kwenye maisha.
Mwanafunzi
wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Manzese anayesoma masomo ya
mchepuo wa sayansi Noela Shirima akielezea kwa waandishi wa habari
namna watakavyonufaika mara utakapokamikika mradi wa gesi asilia
itakayozalishwa na amesema kuwa kujengwa mradi wa gesi na maabara
utawasaidia shuleni hapo kwa manufaa ya kupata elimu bora.
Aidha,
kwa kutambua umuhimu wa uondoshaji wa majitaka, DAWASA iko mbioni
kujenga mitambo yenye uwezo wa kutibu lita milioni 241 za majitaka kwa
siku katika Manispaa zote tatu za jiji la Dar es salaam.
Mitambo
hiyo itajengwa maeneo ya Mbezi Beach (Kinondoni), Jangwani (Ilala) na
Kurasini (Temeke) ambapo wateja wakatakaounganishwa katika mfumo wa
majitaka wataongezeka kutoka 18,568 hadi 25,000 mwaka 2015/2016.
Meneja
wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira
(Biogas) kutoka UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa (kushoto) akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari walipotembelea mradi huo unaotekelezwa
katika shule ya sekondari Manzese mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Majisafi
na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Chakula bora Kata ya Manzes Salehe Rashidi
akielezea kwa waandishi wa habari walipotembelea shule ya sekondari
Manzese mwishoni mwa wiki namna wananchi wake wanavyoshikiana na Uongozi
wa shule hiyo katika kujali taaluma ya wanafunzi na afya zao kwa
kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka shule.
Meneja
Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam
(DAWASA) Bi. Neli Msuya (wa kwanza kulia) akiwaongoza waandishi wa
habari na kujionea sehemu utakapojengwa mtambo wa kuzailsha gesi na
zinapojengwa maabara katika shule ya sekondari Manzese. Kushoto ni
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi
mazingira (Biogas) kutoka UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese wakishiriki kuandaa eneo utakapojengwa mtambo wa kuzailsha gesi shuleni hapo.
Baadhi
wa wananchi wa mtaa wa Chakula bora wakifanya usafi kuzunguka maeneo ya
shule ya sekondari Manzese.(Picha zote na Eleuteri Mangi –MAELEZO).
إرسال تعليق