Wamiliki
wa Skylight Band Dk. Sebastian Ndege na Justine Ndege wakiwa kwenye
moja ya show za vijana wao Skylight Band ndani ya kiota cha maraha Thai
Village Masaki jijini Dar.
Na MOBlog Team
KAMA
ni mpenzi wa muziki hutasita kukubaliana nami kwamba tangu Skylight
Band iingie katika ulimwengu wa muziki wa laivu nchini hapa, kuna mambo
mengi yamebadilika hasa namna ya kutoa burudani hiyo miongoni mwa bendi
ambazo zilikuwapo au tuseme zipo hadi sasa.
Bendi hii ambayo ilianza 2011 imekuwa tishio kutokana na aina yake ya muziki wanayoipiga ya Afro Pop.
Hivi
karibuni kutokana na mafanikio hayo yanayoonekana dhahiri hasa katika
viwanja vya Thai Village na Escape One, Mo Blog ilipata nafasi ya
kuzungumza na Mkurugenzi wa Skylight Band, Justine Ndege ambaye yeye na ndugu yake Dk Sebastian Ndege ndio wamiliki wa bendi hiyo.
Kwenye
mazungumzo hayo na Zainul Mzige wa MOblog ilitaka kujua jinsi wazo la
kuundwa kwa bendi hiyo lilivyofikiwa,uundaji wenyewe ulivyokuwa,
mikakati ya kujitambulkisha na kujua hali ya baadaye ya bendi na
changamoto zake.
Wanamuziki
wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao kwenye uwanja wao
wa nyumbani kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar kila siku ya
Ijumaa wanakuwa hapo kuanzia saa tatu usiku: Kutoka kushoto ni Joniko
Flower, Mary Lucos, Sony Masamba, Aneth Kushaba AK47 na Sam Mapenzi
wakiwajibika jukwaani.
MO BLOG : Naomba kabla ya kuanza kwa mazungumzo jitambulishe kwa wasomaji wetu.
SKYLIGHT: Mimi
naitwa Justine Ndege ni mkurugenzi wa skylight band na Skylight
entatainment. Skylight ni bendi ya ndugu wawili, Dk Sebastian Ndege na
Justine Ndege na wote ni wakurugenzi; sisi ni kaka na mdogo.
MO BLOG :Unaweza kutuambia namna mlivyofikiria kuanzisha bendi hii?
SKYLIGHT: Wazo
la kuanzishwa kwa Skylight Band lilifanyika wakati tukiwa katika
burudani, mimi na ndugu yangu.Tukiwa tunakunywa na kuangalia mambo
yanayoendelea pale.Katika mazungumzo tukasema kuna kitu kikubwa tunaweza
kukifanya kuboresha mazingira kama haya badala ya kunywa na kuzungumza
na marafiki pekee.
Katika mauzngumzo tukasema kwanini tusiwe na bendi ya kuburudisha.
Sehemu
ya wanamuziki wa Skylight Band wakitumbuiza mashabiki wao wakiongozwa
na Meneja wa Bendi hiyo kutoka kulia ni Aneth Kushaba AK47, Digna
Mbepera, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa bongo na Hashim Donode.
MO BLOG: Ilitokea tu wazo la kuwa na bendi au kuna kitu kiliwasukuma?
SKYLIGHT : Ni
wazi kipo kitu kilichotusukuma ndio maana tukawaza. Tulitaka kubadili
mambo katika burudani.Huko nyuma Dk Sebastian Ndege alikuwa anafanya
mambo ya ushereheshaji yaani mc, alikuwa DJ na alikuwa na vifaa vya
muziki.Tukasema basi hebu tujaribu .
MO
BLOG: Mlipoamua kwamba tujaribu nini cha kwanza mlikifanya, mliitisha
vyombo vya habari kama wengine wanavyofanya tunataka hiki?
SKYLIGHT: Ha
ha ha unaenda kasi sana, hapana. kwanza lazima uwe na mtu ambaye unajua
anaweza kutengeneza mambo fulani. Kwa hiyo mtu wa kwanza kabisa
kumfikiria ambaye tulishawahi kufanyanaye kazi alikuwa ni Aneth Kushaba.
Tukamwambia basi tukutane nyumbani kwa Dk Sebastian na akafanya hivyo.
Ndio kusema Skylight iliundwa nyumbani kwa Dk . Sebastian Ndege mwaka
2011.
Pale
Aneth alichukua jukumu la kukusanya.Tukasema hebu Aneth kusanya watu
tuone kama inawezekana. Muziki wa kwanza muziki wa pili tukasema
inawezekana. Tukasema twende kazini kuleta changamoto kwenye muziki wa
laivu.
MO BLOG :Naam mazoezi yamefanikiwa baada ya hapo burudani mliianzishia wapi?
SKYLIGHT: Tulifanya
utafiti wa kutosha, tukajaribu kufuatilia ,tukachekecha kuona tutaanzia
wapi, tukapata sehemu yetu ya kwanza ilikuwa Mafia Fishing Lounge.
Tukaanza pale tukajaribu kuleta mashabiki, tukaweka strategy (mikakati)
tofauti ya kujitangaza. Tukaweka matangazo katika maradio, kwenye
mativii (televisheni) na kwenye Blogs. Kwa matangazo hayo, basi
tunashukuru Mungu tulifika sehemu tukagundua kwamba watu wameanza kulewa
muziki wa laivu na Skylight Band ni kitu gani.
MO BLOG: Inaonekana mambo yenu yanenda poa hamna shida yoyote ukiangalia jinsi watu wanavyowashabikia?
SKYLIGHT: Changamoto
kiukweli zipo lakini mpaka leo tunamshukuru Mungu tumepata mashabiki
kutoka sehemu mbalimbali.Kiukweli chalenge (changamoto) ni nyingi sana
zikiwemo gharama za kuweka wasanii , kuwatunza, kuwapa mishahara
kuwahudumia, lakini tunashukuru Mungu mambo yanaenda vizuri.
MO BLOG: Mambo gani hasa mmejifunza kama menejimenti toka muanze kutoa burudani 2011?
SKYLIGHT: Toka
tumeanza kufanya burudani jambo zuri tumegundua kwamba mashabiki
wanatoka sehemu mbalimbali kila mkoa, kila kata kila sehemu na uzuri ni
kwamba unaweza kusikia jina kubwa la Skylight, lakini ukija kwenye shoo
zetu ambazo tunazifanya kila Ijumaa na Jumapili za public
(zisizobinafsi) kiingilio ni reasonable (kinachowezekana kwa nafasi
yetu kiuchumi). Unaposogea unakuta kiingilio sh elfu 5 Thai village;
unaposogea Escape One unakuta kiingilio sh elfu 7, yote hayo yanatokana
na strategy (mkakati) yetu ya kuleta au kuweka mabadiliko au changamoto
kwenye muziki wa laivu.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akiwajibika jukwaani.
MO BLOG: Kwanini mfikirie kwamba mkakati wenu ndio hasa unaoleta changamoto?
SKYLIGHT: Kwa
sababu mpaka tunaanza kufanya muziki wa laivu na kuweka Skylight Band,
muziki wa laivu ulikuwa kama umeanza kupwaya kidogo kwa Sio tunafikiria
tunaona. Kuna mabadiliko mengi katika muziki wa laivu tuliyoyasababisha.
Bendi nyingi sasa, mathalani zinatumia mitandao ya kijamii kujitangaza.
Sisi tulianza na mkakati wa kujitangaza kwa kutumia mitandao ya
kijamii, tukisema jamani kuna kitu kipya mtaani kuna bendi inaitwa
Skylight. Tukatumia picha, tukatumia maelezo, tunaionesha jamii, nayo
ikatukubali. Ndio maana sasa hivi unaona kweli bendi sasa zinatumia
mitandao ya kijamii. Tunashukuru sana wadau wa mitandao ya jamii,
tunashukuru MOBlog na Zainul Mzige Meneja Mwendeshaji wake,
wametusaidia sana, tuna mshukuru Haki
Ngowi, LeMUTUZ, Jestina George, Global Publishers, Jamii Forum, Michuzi
blog, DJ Sek Blog, DJ Choka, Wavuti, Vijimambo, Sunday Shomari,
Fullshwangwe, Deo Rweyunga, Harakati za Bongo, Josephat Lukaza,
Kajunason Blog, Kamera yangu, Bukoba Wadau, Gsengo, Michuzijr,
Lukwangule Blog na wengine wengi kwa
kuhakikisha kwamba Skylight inapata jina na kufika hapa ilipo. Lakini
pia tunawashukuru mashabiki wameipokea vizuri bendi na wameiweka
Skylight juu.
MO BLOG: Wakati tunafikia mwisho wa mahojiano yetu unaweza kutudadavulia nini mipango yenu ya baadae?
SKYLIGHT: Plani
zetu sisi ni kwenda zaidi, sasa hivi tunakwenda kimataifa tunatafuta
masoko kimataifa kwa sababu tunaamini soko la nyumbani tumefanya
tunachohitajika kufanya, japo yapo mengi tunayotakiwa kufanya.Kwa
kuzingatia strategy yetu tunaamini kuna lengo tumelifikia kwa hiyo
tunataka kwenda kimataifa.
MO BLOG: unaweza kutaja baadhi tu ya mafanikio hayo?
SKYLIGHT: Mengine
tumeshasema kuhusu mashabiki kutukubali lakini ukienda katika medani ya
muziki yenyewe mpaka sasa Skylight band imeshatengeneza nyimbo nane
ambazo zinafiti albamu lakini zile ambazo zipo kwa umma sokoni ni nyimbo
tano na video tano.
MO BLOG: Ningefurahi kama ungeliwatajia watu nyimbo hizo na zingine tatu zipo hatua gani?
SKYLIGHT: Nyimbo
yetu ya kwanza inaitwa “WIVU ambayo ina audio na video , nyimbo yetu ya
pili ni “NASAKA DOUGH” nayo ina video na audio nyimbo yetu ya tatu ni
“CAROLINA” ina audio na video, nyimbo yetu ya nne ni “PASUA TWENDE” na
nyimbo zote zinapatikana katika mtandao wa You Tube. Nyimbo yetu ya tano
inaitwa “MAPENZI GANI” na ipo katika audio na sasa inatengenezewa video
ambayo itakuja .
Sehemu
ya mashabiki wa Skylight Band wakicheza moja ya staili za bendi hiyo
kwenye kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar ambapo kila
Ijumaa bendi hiyo inatoa burudani kwa mashabiki wake.
MO BLOG: Pamoja na kwenda kimataifa nini kingine mmekifikiria huko mbeleni?
SKYLIGHT: Mipango
yetu ya mbeleni ni kuhakikisha kwamba tunafanyakazi kwa kuangalia
soko.Ila tunashukuru kwa Mungu ni kuwa mpaka sasa hivi strategy
tulizozipanga zinaenda sawa tukimaliza ngwe ya kwanza tutaenda ngwe ya
pili.
Projection
(malengo) zetu ndani ya miaka mitano tunataka tuwe Afro Pop and Live
Band, the best in Tanzania (bendi bora ya muziki wa laivu wa pop).Na hii
inaonekana hata namna tunavyoingia kwenye tuzo mbalimbali. Kwa bahati
nzuri au mbaya tumepata nomination (uteuzi) za mtu binafsi katika
tournament za Kili Music na tuzo zingine. Tunaamini mwaka mmoja ujao
tutaingia katika kategori kama bend.
MO BLOG: Unaweza kmunitajia idadi ya wanamuziki na kazi wanayoifanya katika Skylight band?
SKYLIGHT: Jumla
wapo 16 na meneja wa bendi ni Aneth Kushaba. Safu ya waimbaji ni yeye
Aneth Kushaba AK47, yupo Mary Lucos, Digna Mbepera, Joniko Flower, Sam
Mapenzi, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa na Hashim Donode.
Kwenye
vyombo wapo Idrisa (mpiga drum), Baraka (mpiga drum), Emma ( mpiga
bass), Danny Ki (mpiga bass), Tophy (mpiga bass) Amos ( mpiga
kinanda),Daudi (mpiga tumba), Joshua Ngoje (mpiga solo) na Allen Kisso
Mundele (mpiga solo).
MO BLOG: Una neno la mwisho?
SKYLIGHT: Ninalo.Tunawashukuru mashabiki wetu wote, wadau, waandishi wa habari tunaomba waendelee kutusapoti Skylight Band.
إرسال تعليق