Na Keneth Ngelesi wa eddy blog, Mbeya
MWEKAHAZINA
Halmashauri ya Jiji la Mbeya, James Jiorojik (59) na Mkurugenzi wa kampuni ya
uwakala wa kukusanya ushuru ya (DIEMM) Boniface Magessa (38), jana walipandishwa
kizimbani katika Mahakama ya hakimu Mkazi Mbeya kwa makosa ya makosa mnne ya likiwemo
kosa la udanganyifu na kujipatia manufaa binafsi kinyume cha sheria.
Kabla ya kufikishwa
mahakama na Tasisi Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa
Mbeya, iliwalikamata watuhumiwa hao, Oktoba 13 mwaka huu na kushikiliwa katika ya mahabusu
ya polisi kutuo cha kati.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu
wa mahakama hiyo, Michael Mtaite, Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa
Mbeya,Joseph Mulebya, alisema katika
shauri hilo namba 99 la mwaka 2014, washitakiwa kwa pamoja walitenda makosa hayo kwa lengo la kujinufaisha
binafsi.
Mwendesha mashitaka huyo wa TAKUKURU
alisema mahakani hapo kuwa, mshitakiwa
namba moja, ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya (DIEMM), Magessa anahusika na
makosa yote manne, ilhali mweka hazina wa Jiji yeye anashitakiwa kwa kosa moja.
Aliyataja makosa hayo kuwa ni
udanganyifu, kutoza ushuru wa magari kinyume na taratibu, kuhadaa na kukusanya
ushuru kinyume cha sheria, pamoja na kufanya upendeleo kwa lengo la kujipatia
manufaa binafsi.
Alisema mbali na kutoza
ushuru huo, lakini pia Magesa kupitia kampuni hiyo alikuwa akikusanya ushuru wa
magesho katika magari hayo yasiyo ya biashara kinyume kabisa na agizo la
mwajiri wake ambaye ni Halmashauri ya Jiji kama ilivyoelekezwa kwenye sheria
ndogo za Halmashauri hiyo.
Na kwamba
alifanya hivyo , ikiwa ni kinyume cha sheria ya adhabu namba 304, kifungu cha 16 na marekebisho yake
ya mwaka 2020 na ile ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 11 ya mwaka 2007
.
Wakati
shitaka la nne liliwahusu washitakiwa wote wawili la kufanya udanganyifu na
upendeleo , ikiwa ni kinyume cha sheria namba 15(i)(a) ya kuzuia na kupambana
na rushwa sura ya 11 ya mwaka 2007 .
Washitakiwa hao wote wanaotetewa na wakili, Ladslaus Rweikaza,
walikana mashitaka hayo wako nje kwa dhamana na kesi hiyo
itaendelea Oktoba 23 mwaka huu.
Hata hivyo,
kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa ilitawaliwa na vituko, ambapo eddy blog ilishuhudia baada ya
watuhumiwa kufikishwa mahakamani hapo, mshitakiwa namba mbili ambaye ni
Mwekahazina wa Jiji la Mbeya alionekana kuweweseka.
Mwekahazina
huyo aliyeonekana kupagawa alisikika akiwaambia maofisa wa Takukuru
waliomfikisha mahakamani hapo wamwache akamalizie kazi zake.
Mweka hazina
huyo alikaririwa akisema wamwache kwanza akasaini mafaili, ‘ niacheni nika
saini mafaili ….liko wapi lile faili na zile LPO,, hali iliyoibua vicheko kwa
watumishi wenzake waliokuja kumpa pole na kusikiliza kinachooendelea.
إرسال تعليق