Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Thomasi Kashililah.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Thomasi Kashililah
anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri kuwa Vikao
vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza Jijini Dar es Salaam tarehe 20
Oktoba 2014. Kwa tangazo hili waheshimiwa Wabunge wote mnaombwa kuwasili
Dar es Salaam siku ya Jumapili tarehe 19 Oktoba 2014.
Kamati
za Bunge katika vikao hivi vitakavyodumu hadi tarehe 2 Novemba 2014
zitapokea na kujadili pamoja na mambo mengine Muswada wa Marekebisho ya
Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2014,
Kukagua miradi mbalimbali, kutembelea Mamlaka ya Bandari, Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo na kujadili Sheria ya VAT katika muktadha wa Sekta
ya Elimu nchini. Pia zitapokea taarifa kuhusu Sheria ya mazingira
inavyotekelezwa katika migodi ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, na North
Mara, pamoja na kuijadili kwa ujumla taarifa ya CAG kuhusu ukaguzi wa
Hesabu za Serikali Kuu na mashirika ya umma kwa mwaka 2013.
Aidha
kutakuwa na maoni ya wadau kuhusu muswada ya Sheria ya Baraza la Vijana
wa mwaka 2013 na kupokea taarifa kuhusu migogoro ya mipaka kati ya
Hifadhi za taifa za Saadani, Manyara, Tarangire, Mikumi, Ngorongoro,
Ruaha na vijiji vinavyopakana na Hifadhi hizo.
Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam,
18 Oktoba 2014
إرسال تعليق