Huku
gharama ya ardhi ikizidi kupanda, baadhi ya maeneo yaliosahaulika kama
vile vyoo vya zamani yamegeuzwa na kufanywa kuwa migahawa na maduka ya
kuuza nguo.
Vyoo vingi vya kukojoa vilisahaulika kwa miongo kadhaa
baada ya vita vya dunia vya pili ,lakini kufuatia hatua ya maafisa wa
jiji hilo la kutaka kupata mapato, mabadaliko hayo yanafanyika kwa kasi.Baadhi ya migawaha hiyo ni 'The Convinience' uliofunguliwa katika eneo la Hackney mwaka 2013, 'WC' ambalo ni duka la mvinyo lililopo katika eneo la Clapham kusini mwa London na 'ArtsLav' ambalo ni eneo la maonyesho lililopo katika eneo la Kennington.
Kulingana na mtandao wa gazeti la daily Nation nchini kenya, Maeneo mengine yaliokuwa vyoo na kugeuzwa ni 'the Attendant' na 'the Cellar Door' cabaret lililopo katikati ya mji wa London.
Mwenendo huo ulianza hivi majuzi kulingana na Rachel Erickson ambaye kazi yake ni kupanga mipango ya watalii kuzuru katika vyoo hivyo hatua iliomsababisha kuitwa 'Mwanamke wa vyoo'.
Jayke Mangio mwenye umri wa miaka 34,ambaye alifungua 'WC' mnamo mwezi July,amesema kuwa serikali imekuwa ikilishinikiza baraza la jiji kutumia maeneo yote yalio wazi kuleta mapato.
Baadhi ya maeneo ambayo yamevutia wawekezaji ni vyoo hivyo vya zamani na barabara za chini za treni.
إرسال تعليق