BAADA YA DIAMOND KUDAI MIMBA ALIZOMPA PENNY ZILIHABIKA KIUTATA! ...PENNY AFUNGUKA KIIVI

 Penniel Mwingilwa.
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.

Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa Siku ya (Alhamisi) na gazeti la Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha. 
Akizungumza nasi hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na 


kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi. 

“Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny

Post a Comment

أحدث أقدم