![]()
ASKARI wa jeshi la ulinzi wa Tanzania wakiongoza viongozi wa
serikali ya Tanzania,DRC na viongozi na wananchi wa kijiji cha Kalilani
katika mazishi ya raia 14 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
waliofariki katika ajali ya meli Desemba 12 mwaka huu katika Mkoa Kalemie DRC na
miili yao
kukutwa katika hifadhi ya Taifa ya Mahale.
|
Miili ya watu 14 imezikwa baada ya mashauriano ya serikali za Tanzania na DRC ambapo serikali ya DRC iliwakilishwa na Balozi mdogo wa nchi kutoka Ubalozi mdogo mkoani Kigoma.
Akizungumza muda mfupi kabla ya mazishi ya raia hao,Balozi Mdogo wa DRC katika ubalozi mdogo wa mkoa Kigoma,Riki Moleme alisema kuwa amefarijika
kwa namna serikali ya Tanzania ilivyochukulia kwa umuhimu mkubwa maafa ya Raia hao wa DRC na namna ilivyojitoa katika kushughulikia mazishi ya miili
hiyo.
Awali Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Mahale,Herman Batiho alisema kuwa walianza kuona miili ya watu hao kuanzia majira ya jioni Desemba 20
mwaka huu na ndipo wakaanza kuwasiliana na mamlaka mbalimbali ambapo waliwasiliana na uongozi wa kijiji cha Kalilani ambapo uongozi na wananchi
wa kijiji hicho walianza kusaidia katika kuopoa miili hiyo.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kalilani,Songoro Saidi alisema kuwa waliona mwili wa moja ya maiti hizo asubuhi ya Desemba 21 ambapo pia walipata
taarifa ya kuwepo kwa miili mingine ndani ya hifadhi ya Mahale na ndipo waliposhirikiana na kuiopoa miili hiyo hadi kufanikisha mchakato wa mazisho.
Desemba 12 mwaka huu jumla ya 128 walifariki dunia na wengine zaidi ya 250 waliokolewa kufuatia meli waliyokuwa wakisafiria iliyokuwa ikitoka Moba
kuelekea Kalemie ilizama katika mwambao wa ziwa Tanganyika katika mkoa Kalemia nchini DRC.

إرسال تعليق