Tamasha hilo la wafalme ambalo limeanza kuwa gumzo
la jiji kutokana na kuwa na burudani za aina mbalimbali kwa ajili ya
kukonga nyoyo za wapenzi wa burudani limedhaminiwa na kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,
Matina Nkurlu alisema Vodacom imeamua kudhamini tamasha hilo kwa ajili
ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na wananchi kwa ujumla
katika msimu huu wa sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
“Kama ilivyo kaulimbiu yetu kuwa ‘ukiwa na Vodacom
maisha ni murua’, tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja
wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani, hivyo
ndiyo maana tunadhamini matamasha ya aina hii na tutaendelea kufanya
hivyo siku zote.”
Post a Comment