Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14
yanaonyesha kuwa CCM imefanikiwa kupata ushindi wa jumla mitaa na vijiji
9,406, huku vyama vingine vya upinzani, vimegawana nafasi 3,211.
Hata hivyo, kwa ushindi huo upinzani umeongeza
viti 1,981 ikilinganishwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita,
ambao kwa ujumla, ulipata nafasi 1,230 za wenyeviti wa mitaa na vijiji.
Kwa upande wake, CCM imepoteza nafasi 2,636 za
uenyekiti wa vijiji na mitaa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009
ilipopata jumla ya viti 12,042.
Uchaguzi wa mwaka huu, umefanyika kukiwa na nyongeza ya mikoa, wilaya, mitaa na vijiji katika baadhi ya maeneo nchini.
CCM imepata vijiji 7,290 kikifuatiwa na Chadema
yenye vijiji 1,248. CUF imeshika nafasi ya tatu kwa kuwa na vijiji 946,
ikifuatiwa na UDP yenye vinne na TLP na NLD vyenye viwili kila kimoja.
Katika nafasi za wenyeviti wa mtaa, CCM kimechukua
jumla ya mitaa 2,116. Vyama vingine na nafasi zao kwenye mabano ni
Chadema (753), CUF (235), ACT (9), NCCR - Mageuzi (8) wakati vyama vya
TLP, UMD, UDP na NRA vimepata mtaa mmoja kila kimoja.
Ushindi huo unaotajwa kuwa ni mdogo ikilinganishwa
na ule wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2009 unaonekana kuwa na
maana kubwa kwa chama tawala CCM, hasa katika maeneo ambayo wanatokea
wabunge wake ambao wanatajwa kutaka kuwania urais mwaka 2015.
Moja ya hoja za wagombea urais watakazotumia
kujipigia debe au kuponda wapinzani waoni kwanza kukubalika kwenye
majimbo yao ya ubunge, jambo ambalo pia ni ishara wamekipigania vipi
chama kwenye maeneo yao kabla ya kuomba kupewa dhamana kubwa zaidi ya
kuongoza nchi mwaka 2015
Wanaotajwa kuutaka urais ni Waziri Mkuu Mizengo
Pinda ambaye anatokea jimbo la Katavi, Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa (Monduli), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
Steven Wasira (Bunda), Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe (Mtama).
Wapo pia aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na
Madini, William Ngeleja (Sengerema), Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba (Bumbuli).
Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Dk Emmaniel Nchimbi
(Songea Mjini), Dk Hamisi Kigwangalla (Nzega), Mwigulu Nchemba (Iramba
Magharibi), Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki) na Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela).
Profesa Tibaijuka (Muleba Kusini)
إرسال تعليق