
Katibu
mpya wa Yanga Dk. Jonas Tiboroha, ametangaza mikakati yake ya
kuhakikisha Yanga inajiendesha kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupitia upya
mikataba yote ya wadhamini.
Akizungumza
Makao Makuu ya Klabu hiyo leo, Tiboraha alisema kuwa Yanga ni klabu
kubwa hiyo ni wakati wa kujiendesha yenyewe badala ya kutegemea mtu
binafsi na kwamba haiwezi kuwa na mikataba ambayo haikithi maslahi ya
klabu hiyo.
"Yanga
ni bidhaa inayojiunza yenyewe uwezi kuingia mkataba wake sawa na Stand
United, haiwezekani ikapata mgao sawa kama wanafunzi wa shule ya msingi
unawapanga mstari unawambia haya kila mtu unamgawia pipi moja moja na
wanaridhika, haiwezekani ni lazima Yanga iwe tofauti.
"Klabu
kama Liverpol, inawashabiki wengi hata kama haipo kwenye nafasi nzuri
kwenye msimamo wa ligi linapokuja suala la mgao wa fedha inapata fungu
kubwa kwa vile tayar inajiuza, sasa Yanga ingie mikataba sawa na kina
Stand United dunia nzima itatushangaa."alisema.
Alisema
sekreatrieti mpya ambayo wanaiongoza ipo kwenye mchakato wa kupitia
upya mikataba ya TBL, Vodacom na Azam ambayo hadi sasa klabu hiyo ya
Jangwani imesusia fedha zake wakidai nyongeza kwa vile hawawezi pata
mgao sawa na timu nyingine.
Hata
hivyo Tiboraha ambaye ni mwana Falsafa wa Michezo, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), alisema mpira wa Tanzania umegubikwa na changamoto kubwa
na kwamba miezi minne aliyofanya kazi Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), amegundua Yanga kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi
ili iweze kutoka hapo ilipo na kusonga mbele.
"Katika
maisha yangu ya mpira dunia, hakuna timu inayoendelea bila kujenga uwzo
binafsi, lazima tujenge uwezo wa timu kujiendesha yenyewe kimaslahi,
kuwekeza kwa vijana wadogo nitahakikisha nalisimamia hilo.
"Klabu
za Tanzania sio Yanga tu, zimekuwa na utamaduni wa kukimbilia kusajili
wachezaji kwa mamilioni, garama kubwa wakati wangewekeza kwa vijana hata
timu ya Taifa ingekuwa bora na tungefanya vizuri kwenye michuano mbali
mbali ya kimataifa.
"Mfano
Msuva (Simon) nilimfundisha mimi, mazoezi alikuwa akifanyia pale UDSM,
niliwambia Yanga mchukueni huyu kijana, wakadengua akachukuliwa na timu
nyingine matokeo yake Yanga wamekuja kumsajili kwa gharama kubwa."
"Ligi
ya Tanzania ni dhaifu, nikikumbuka wakati mdogo klabu kama yanga ilikuwa
na timu A mpaka C, wachezaji wanakuzwa na ndio waliowika siku za nyuma
lakini sasa hivi tunakimbilia kusajili wachezaji wa nje kwa garama
kubwa, wengine ndio unakuta klabu zinaingizwa mkenge kwa kusajili
wachezaji bomu kwa vile hawawajui.
"Mabadiliko
natakas yaanzie Yanga, klabu zikijenga utaratibu huu hata Ligi itakuwa
imara na hazitakimbilia kusajili wachezaji wa nje, chukulia mfano Azam
ina kila kitu lakini ukiangalia 'quality' walionao hawaendani na
uwekezaji uliofanywa.
"Kwa
hapa nchi tunasema Azam klabu bora kwa vile msimu uliopita imecheza
mechi zote bila kufungwa, lakini hiyo haitoshi kusema ni bora, utasema
bora kama italeta ushindani kwenye michuano ya kimataifa sio inacheza
raundi ya kwanza ya pili inatolewa, uwezi ifunga Stand United bao tatu
ukajisifu wewe bora, kama unaweza kuifunga tatu, ikicheza na Esparance,
TP Mazembe au Motemapembe itafungwa 18, kwa sababu 'quality' ya
wachezaji Tanzania bado sana, tunataka Yanga ianze kuwa mfano.
Katika
hatua nyingine, Tiboraha alisema kuwa hana wasiwasi na kutimuliwa Yanga
iwapo uwezo wake utaonekana mdogo kutoka na historia ya klabu hiyo
ambayo ndani ya miaka miwili chini ya mwenyekiti Yusuf Manji
wameshafungashiwa virago makatibu watatu akiwemo Laurance Mwalusako,
Selestine Mwesigwa ambaye ameuburuza uongozi huo mahakamani pamoja na
Benno Njovu ambaye nafasi yake imechukuliwa na Tiboraha.
"Nimejiandaa
kwa lolote ninachofahamu wengine mikataba yao imeisha ndio maana
wameondoka wengine hawajaperfome, hata mimi kama sina onyesha uwezo nipo
tayari kuwajibika."
إرسال تعليق