Nguli wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ akiwa na Kajala Masanja.
Stori: Deogratius Mongela NGULI
wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ amefunguka kuwa,
mastaa wengi wa kike wamemgeuza babu yao kwa kumfanyia vituko kila
wanapokutana naye.Akitema mbili tatu na paparazi wetu baada ya kusambazwa kwa picha mtandaoni inayomuonesha akifanyiwa vituko na staa mwenzake, Kajala Masanja, Mzee Majuto alisema watu wasimfikirie ndivyo sivyo kwani yeye wasanii wengi wa kike wamemgeuza babu yao.
Mzee Majuto akiwa na Odama.
“Wasanii wengi wamenizoea sana, huwa wananitania mara kwa mara na
miye nawachukulia kama wanangu hasa hawa mastaa wa kike tofauti na
wanaume, sijawahi kuwa na uhusiano na staa yeyote kati yao,” alisema
Mzee Majuto.
إرسال تعليق