Hali hiyo lisibabisha wafuasi wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao walifurika kwenye kituo cha
kupigia kura kilichopo Mtaa huo, kupinga matokeo hayo kwa madai kuwa
hawajapiga kura iweje matokeo yatangazwe.
Hatua hiyo ilisababisha Polisi kuingilia kati
kuwatawanya wafuasi hao kwa kupiga mabomu ya machozi, jambo ambalo
lilisababisha wafusi hao kutawanyika sambamba na wananchi waliyojitokeza
kupiga kura.
Wakati hayo yakitokea Mbunge wa Ilemela, Highnes
Kiwia alimsimika mgombea wa Chadema, Ramadhani Saidi kuwa Mwenyekiti wa
Mtaaa huo, kwa madai kwamba ndiye chaguo la wakazi wa Mtaa huo na kwamba
hawawezi kuchagulia kiongozi wasiyomtaka.
Kiwia alisema, “Haiwezekani watu wamejitokeza
kupiga kura, wanakuta matokeo tayari yamebandikwa, ni jambo la ajabu na
lakushangaza watu hawajapiga kura matokeo yanapatikanaje, lazima suala
hilo litolewe ufafanuzi wa kina.”
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta
msimamizi wa uchaguzi huo Wilaya ya Ilemela ambaye ni Kaimu Mkurugenzi
wilaya hiyo, Justin Lukaza, na kueleza kwamba matokeo hayo ni sahihi,
kwani uchaguzi wa Disemba 14 walishindwa kutangaza matokeo kutokana na
tofauti zilizotokea, hivyo leo wameamua kuyatoa.
Akizungumza na mwandishi wa gazeiti hili Katibu wa
Chadema tawi la Ibungilo B, Abedi Bulashi alisema kuwa uchaguzi
ulifanyika Disemba 14, ulimalizika usiku wa manane, lakini kulitokea
kasoro na msimamizi wa uchaguzi huo aliharisha uchaguzi na kupanga
kurudiwa leo (jana).
Mmmo ya wananchi yao Daniel Buzuka alisema, “Mimi
nilifika asubuhi hapa kituoni kupiga kura, lakini nilishangaa kuona
polisi wanakuja na kusema hakuna uchaguzi, huu ni ubabe umetumika na
wametunyima haki yetu ya masingi
إرسال تعليق