Miss
Tanzania 2013, Hapopiness Watimanywa (kushoto) amerejea hii leo
akitokea jiji London Uingereza alikokuwa akishiriki mashindano ya Miss
World 2014.
Watimanywa
akizungumza na Father Kidevu Blog hii leo asubuhi baada ya kuwasili
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Kupokelewa na Miss
Tanzania 2014, Lilian Kamazima (Pichani kulia), Viongozi wa Kamati ya
Miss Tanzania pamoja na familia yake alisema kuwa licha ya kuwa yeye
hakufanya vyema katika mashindano hayo lakini amefurahi taji hilo kuja
Afrika.
Aidha
Watimanywa amewaasa warembo wenzake hasa Lilian Kamazima anaetaraji
kwenda katika mashindano hayo mwakani kutumia zaidi kujichanganya katika
mitandao ya kijamii kama facebook, Twitter na Instagram ili kujipatia
kura nyingi hapo baade.

Happiness akilakiwa na wadogo zake Angela Roussos na Romeo baada ya kuwasili hii leo asubuhi.

Happiness akipokelewa mizigo na baba yake, Lous Rousso.

Mkurugenzi wa Lino Intenational Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga akimsalimia Happiness Watimanywa. Kulia ni baba yake, Lous Rousso

Happiness Watimanywa akiwa na Mama yake Amina Bukoko.

Happiness akizungumza na familia yake uwanjani hapo.
Picha ya pamoja ya wote waliofika kumpokea Happiness Watimanywa.Picha Na Father Kidevu
إرسال تعليق