| Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesigwa Lukaza wakiwa mahakamani wakisubiri hukumu |
Akitoa hukumu hiyo jana Kiongozi wa jopo la
Mahakimu watatu wanaoisikiliza kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Edson
Mkasimongwa alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi
saba wa upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa hao anaona upande wa
mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka.
Mashtaka matano yaliyokuwa yakiwakabili hao ni
pamoja kula njama, kughushi, kuwasilisha hati za uongo za makubaliano ya
kuhamisha deni kati ya kampuni yao ya Kernel Ltd na kampuni Marubeni
ya nchini Japan na kujipatia kiasi hicho cha fedha cha Sh 6.3 bilioni
kwa njia ya udanganyifu.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mkasimongwa amesema
wamewaachia huru washtakiwa hao katika makosa hayo yote kwa sababu
ushahidi wa upande wa mashtaka haukujitosheleza kwa kuwa ulishindwa
kuthibitisha kama ni kweli Novemba 2,2003 washtakiwa hao walighushi
hati ya makubaliano ya kuhamisha deni la Sh 6.3 bilioni baina ya
kampuni ya Kernel Ltd na Marubeni ya nchini Japan ilikuwa ni ya
kughushi.
Jaji Mkasimongwa anasema ushahidi unaonesha
kampuni hiyo ya Marubeni ya nchini Japan ilikubali kupokea kiasi hicho
cha fedha na kwamba washtakiwa wao walipata asilimia tu ya 20 ya
fedha hizo na upande wamashtaka hakuwahi kulibishia hilo.
Katika kesi hiyo, Johnson Lukaza ambaye ni
Mwenyekiti wa makampuni ya Proin na ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu
cha Bagamoyo (UB) pamoja na mdogo wake Mwesiga walikuwa wanatetewa na
Wakili Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa ndugu wa washtakiwa
hao waliaza kulia mahakamani hapo pamoja na mshtakiwa Mwesiga wakiwa
hawa amini kilichotokea huku wakisema asante Yesu, asante Yesu.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق