Mtandao
wa Korea kazkazini ulizimika kwa masaa kadhaa na kuzua uvumi kwamba
huenda Marekani imeanza kulipiza kisasi kufuatia madai ya uhalifu wa
mtandaoni uliofanyiwa kampuni moja ya filamu nchini Marekani.
Kulingana
na kituo cha habari cha AFP haijulikani ni nani ama nini kilichozima
mtandao wa Pyongyang ,lakini wataalam wa mitandao wamesema kuwa mtandao
wa taifa hilo ulizima usiku kucha kutoka siku ya jumatatu hadi jumanne.Kampuni ya Dyn Research imesema kuwa mitandao michache iliopo Pyongyang huenda ikaathiriwa na kukatika kwa umeme lakini vile ilivyozimika kunazua mjadala kwamba huenda mitandao hiyo ilizimwa kutoka nje.
Maafisa wa Washington wamekataa kutoa tamko kuhusu madai kwamba kuzimwa kwa mtandao wa Korea Kazkazini ni hatua ya kwanza ya rais Obama aliyeonya kwamba atalipiza kisasi shambulizi hilo.
Post a Comment