Polisi na Sumatra wafanya ukaguzi wa kushtukiza wa mabasi ili kupunguza ajali Shinyanga.

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) mkoani Shinyanga limefanya ukaguzi wa kushitukiza ili kuwabaini madereva walevi wa mabasi  yaendayo mikoani na mawilayani kwa lengo la kupunguza ajali zinazotokana na uzembe katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho wa mwaka.
Ukaguzi huo wa kushitukiza ulioambatana na ukaguzi wa nauli halisi na uchafu wa mabasi umefanyika katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Kahama ambapo mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoani hapa Bw. Desdery Rugimbana amewataka abiria wanaosafari na mabasi hayo kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wanapoona dereva akienda kwendo kasi, kukiuka sheria za usalama barabarani  au akitumia kilevi chochote wakatia akiwa anaendesha.
 
Kwa upande wao baadhi ya madereva na abiria wa mabasi hayo ambayo mengi hufanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Geita, Kagera, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Msumbiji, Rwanda na Uganda wameliomba jeshi la polisi kuweka mpango mkakati wa kufanya ukaguzi huo kuwa endelevu walau mara tatu kwa wiki badala ya kulifanya wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka hali itakayosaidia kupunguza ajali za barabarani na kuokoa maisha ya watu.
- ITV

Post a Comment

Previous Post Next Post