Jeshi
la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na mamlaka ya
udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) mkoani Shinyanga
limefanya ukaguzi wa kushitukiza ili kuwabaini madereva walevi wa mabasi
yaendayo mikoani na mawilayani kwa lengo la kupunguza ajali
zinazotokana na uzembe katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho wa
mwaka.
Ukaguzi huo wa kushitukiza ulioambatana na ukaguzi wa nauli halisi
na uchafu wa mabasi umefanyika katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini
Kahama ambapo mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoani hapa Bw.
Desdery Rugimbana amewataka abiria wanaosafari na mabasi hayo kutoa
taarifa kwa jeshi la polisi wanapoona dereva akienda kwendo kasi,
kukiuka sheria za usalama barabarani au akitumia kilevi chochote
wakatia akiwa anaendesha.
Kwa upande wao baadhi ya madereva na abiria wa mabasi hayo ambayo
mengi hufanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Geita, Kagera, Kigoma,
Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Msumbiji, Rwanda na Uganda
wameliomba jeshi la polisi kuweka mpango mkakati wa kufanya ukaguzi huo
kuwa endelevu walau mara tatu kwa wiki badala ya kulifanya wakati wa
sikukuu za mwisho wa mwaka hali itakayosaidia kupunguza ajali za
barabarani na kuokoa maisha ya watu.
- ITV
إرسال تعليق