Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya saa 6.45 mchana na
kumalizika saa 8, imesababisha usumbufu mkubwa kwa maelfu ya wakazi wa
jiji la Mwanza ambao walikuwa wakifanya manunuzi ya nguo na vyakula kwa
ajili ya sikukuu ya Krismasi, baada ya maduka yote pamoja na njia za
waenda kwa miguu katika mtaa huo wa makoroboi kujaa maji, hali ambayo
imetibua furaha ya wakazi wa jiji la Mwanza wanaojiandaa kusherehekea
sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo mfalme zaidi ya miaka 2000 iliyopita
huko bethlehemu.
kabla ya mvua hiyo kunyesha, ITV ilipita katika mitaa mbalimbali
ya jiji hili na kukuta baadhi ya wananchi wakiendelea na manunuzi ya
nguo, vyakula na mapambo ambapo katika mtaa wa Makoroboi uliopo katikati
ya jiji la Mwanza hali ilikuwa hivi.
إرسال تعليق