Someni ili mnufaike na gesi, mafuta

Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tatu nchini Qatar na kazi kubwa ni kutafuta wawekezaji katika sekta ya mafuta na gesi wananchi mkoani lindi wamehimizwa kusoma ili waweze kuzitumia vyema fursa zitakazotokana na rasilimali hizo.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa chuo kikuu Huria cha Tanzania Tawi la Lindi,Dk Irene Tarimo kwenye hafla ya kumuaga makamu mkuu wa chuo kikuu hicho taifa,Profesa Tolly Mbwete iliyofanyika mjini Lindi.
Dk Tarimo anasema wananchi katika mkoa huu hawanabudi kusoma kwa bidii ili pamoja na mambo mengine waweze kufaidika na fursa zinatokana na mafuta na gesi asilia iliyogunduliwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Anasema itakuwa ni vigumu wananchi wa mkoa kufaidi na fursa zitakazotokana na ugunduzi wa maliasili hizo iwapo wataendelea kuwa nyuma  kielimu.
Anabainisha kuwa utafiti uliofanywa mwaka 2010 umeonyesha kuwa 5% tu ya wenyeji wa  mkoa huo ndio wanaosoma katika chuo hicho na asilimia 95% wanatoka nje ya mkoa huo.
“ Unajua ndugu zangu, mwanamke akiwezeshwa anaweza, tena ni watu muhimu sana katika jamii zetu, ninatoa wito kwa wanawake kujiandikisha kwa wingi chuoni hapa ili wawe chachu ya maendeleo katika mkoa wetu.”anasema Dk Tarimo
Anasema siku zote elimu humkomboa mtu yeyote, hivyo aliwasi wananchi wa mtwara kutoionea haya elimu, wawekeze kwenye elimu ili siku moja waje kuona faida ya kusoma na kusomesha

Post a Comment

Previous Post Next Post