Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anaendelea na ziara yake
ya siku tatu nchini Qatar na kazi kubwa ni kutafuta wawekezaji katika
sekta ya mafuta na gesi wananchi mkoani lindi wamehimizwa kusoma ili
waweze kuzitumia vyema fursa zitakazotokana na rasilimali hizo.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa chuo kikuu
Huria cha Tanzania Tawi la Lindi,Dk Irene Tarimo kwenye hafla ya kumuaga
makamu mkuu wa chuo kikuu hicho taifa,Profesa Tolly Mbwete iliyofanyika
mjini Lindi.
Dk Tarimo anasema wananchi katika mkoa huu
hawanabudi kusoma kwa bidii ili pamoja na mambo mengine waweze kufaidika
na fursa zinatokana na mafuta na gesi asilia iliyogunduliwa katika
mikoa ya Lindi na Mtwara.
Anasema itakuwa ni vigumu wananchi wa mkoa kufaidi
na fursa zitakazotokana na ugunduzi wa maliasili hizo iwapo wataendelea
kuwa nyuma kielimu.
Anabainisha kuwa utafiti uliofanywa mwaka 2010
umeonyesha kuwa 5% tu ya wenyeji wa mkoa huo ndio wanaosoma katika chuo
hicho na asilimia 95% wanatoka nje ya mkoa huo.
“ Unajua ndugu zangu, mwanamke akiwezeshwa
anaweza, tena ni watu muhimu sana katika jamii zetu, ninatoa wito kwa
wanawake kujiandikisha kwa wingi chuoni hapa ili wawe chachu ya
maendeleo katika mkoa wetu.”anasema Dk Tarimo
Anasema siku zote elimu humkomboa mtu yeyote,
hivyo aliwasi wananchi wa mtwara kutoionea haya elimu, wawekeze kwenye
elimu ili siku moja waje kuona faida ya kusoma na kusomesha
إرسال تعليق