Uda yanusuru wasafiri kwenda Kilimanjaro

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetoa vibali 15 vya mabasi ya Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (Uda) kwa lengo la kusafirisha abiria kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Kilimanjaro wa kati wa sikukuu.
Vibali hivyo vilitolewa kwa ajili ya Krismasi na  Mwaka Mpya kutokana na matatizo ya usafiri wa kwenda katika mkoa huo.

Mkurugenzi wa Sumatra, Gilliard Ngewe, aliliambia NIPASHE jana kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya abiria kuwa wengi na mabasi kuwa machache katika Kituo Kikuu cha Mbasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Ubungo (UBT), hivyo kushindwa kusafirisha abiria wote.

“Tumeangalia namna ya kuweza kuwasafirisha abiria wote waliofika kituoni hapa, tukaona ni lazima tupate usafiri wa ziada, tumeomba mabasi mengine yapeleke abiria Kilimanjaro, lakini bado ikawa haitoshi,” alisema Ngewe.

Alisema baada ya kuzungumza na Uda wakakubali kupeleka usafiri, hivyo wakawa na uhakikia wa kusafirisha abiria wote.

Msemaji wa Uda, George Maziku, alisema wameamua kufanya hivyo baada yakupokea maombi ya serikali ya kupunguza adha ya usafiri  kwa mikoa ya kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga  kwa kipindi cha sikukuu.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni, Awadhi Haji, alisema wanafurahi kutokana na zoezi hilo kufanikiwa kupunguza adha ya usafiri katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post