Shirika
la Viwango Tanzania (TBS), limekifunga kiwanda cha U Fresh kilichopo
Tegeta, jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kutengeza juisi ambazo
zipo chini ya viwango vya ubora.
Shirika hilo limechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa juisi hiyo ina vimelea vya wadudu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Viwango Mwandamizi TBS, Selemani Banza, alisema kuwa baada ya kuzipimia bidhaa hizo wamebaini kuwa na vimelea vingi vya wadudu ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka minane.
Alisema mazingira ya kiwanda hicho ni machafu ndio maana yamesababisha juisi hizo kuonekana na vidudu vingi.
Banza alisema kiwanda hicho kimepewa kibali cha TBS, lakini matokeo yake kinazalisha bidhaa ambazo hazipo chini ya kiwango.
Alisema awali walisema wanatumia sukari tamu, lakini walikatazwa kutumia kwa kuwa ina madhara kwa watoto watakaotumia juisi hizo.
Hata hivyo, alisema kiwanda hicho kilikiuka makubaliano na matokeo yake kikaendelea kutumia sukari tamu badala ya sukari ya kawaida waliyokubaliana kitumie.
Alisema sukari inayotimiwa ina madhara kwa watoto kwa kuwa wanaweza kupata ugonjwa wa saratani pamoja na matatizo ya utindio wa ubongo.
Banza alisema amekifungia kiwanda hicho mpaka hapo atakapotekeleza maagizo hayo na kwamba bidhaa hizo ambazo zipo sokoni wananchi wanatakiwa kuacha kuzinunua.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano cha TBS, Roida Andusamile, alisema sheria namba mbili ya mwaka 2009 inaeleza kuwa endapo mtu akikiuka utaratibu huo atatakiwa kulipa faini ya Sh. milioni 50 hadi 100 au kwenda jela miaka miwili.

CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment