Aliyekuwa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Ludovick Utouh amesema mihimili mitatu ya nchi ambayo ni Bunge, Mahakama
na Serikali isipofanya kazi bila kuangalia mipaka yao kwa mujibu wa
sheria nchi haitatawalika.
Amesema utendaji wa siku kwa siku wa mihimili hiyo
unatakiwa kupimwa kwenye mizani ili kila mhimili ufanye kazi bila
kuingilia kazi za mihimili mingine kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia
kulinda amani ya nchi pia kuongeza utawara bora na wenye maadili mema.
Utouh ameyasema haya leo jijini Dar es Salaam
katika hafla ya kupokea tuzo ya uadilifu na utawala bora kutoka kwenye
kampuni ya Dream Success Enterprises baada kuutambua umuhimu wa
utendaji kazi wake akiwa kazini kabla ya kustaafu.
Amesema ubabe na kutoelewana huku kila mhimili
ukitaka kujiona kuwa upo juu ya muhimili mwingine kuna weza kukaleta
machafuko makubwa yatakayoigharimu nchi, na kwamba kurudisha amani
itachukua muda.
“Kuna haja ya hiii mihimili kufungiwa mizani,
kufanya kazi kwa kutoingiliana, pia ikiheshimiana na kutatua mambo yao
kwa hekima Tanzania itakuwa sehemu tulivu, yenye amani na kimbilio la
wanyonge, lakini kama kila muhimili ukifanya kazi kivyake bila
kuzingatia sheria machafuko yanaweza kutokea na kuifanya nchi
isitawalike,”anasema Utouh.
Anasema katika harakati zake akiwa kazini
atalikumbuka daima sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya nje
(EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa katibu Mkuu wa Nishati na Madini
David Jairo.
Anasema hayo yote yaliwezekana kufanyika kwa
sababu mihimili ya Serikali ilikuwa ikifanya kazi zake kwa weledi wa
hali ya juu bila kuingiliana katika maamuzi.
Anasema tuzo aliyopata anaipokea ingawa katika
kipindi chake cha kazi ndipo kulipozaliwa jina la ufisadi, hata hivyo
amesema anajivunia kuwepo kwake katika ofisi ya CAG kwani alifanikwia
kurudisha imani ya chombo hicho kwa wananchi na hivi sasa wananchi
wanakiamini
إرسال تعليق