Wanawake madereva waingia mashakani saudia
Wanawake wawili wa Saudi Arabia waliokamatwa kwa takriban mwezi mmoja
kwa kukiuka marufuku ya wanawake kuendesha magari nchini humo
wamepelekwa katika mahakama inayosikiliza kesi za ugaidi.
Mawakili wa wanawake hao wamekataa rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Mmoja
wao Loujain Hathloul alikamatwa baada ya kujaribu kuendesha gari
kuingia katika ufalme huo kutoka umoja wa milki za kiarabu.
Maysaa Alamoudi mwandishi kutoka milki za kiarabu aliwasili katika mpaka huo kumsaidia Hathloul na ndiposa akakamatwa.
Baadhi
ya watu wa karibu wa wanawake hao wawili wanasema kuwa wanashtakiwa sio
tu kwa kukiuka marufuku hiyo bali kwa maoni yao walioweka katika
mitandao.
إرسال تعليق