
IDARA
ya Uhamiaji mkoani Geita imewaonya wamiliki wa kumbi za starehe kuacha kuajili
wasanii kutoka nje ya nchi bila kufuata taratibu za uhamiaji hali ambayo ni
kinyume cha sheria za nchi.
Onyo
hilo limetolewa leo na Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Geita,Kamishina Msaidizi
Mwandamizi,Charles Washima,wakati akiongea na kipindi hiki mara baada ya
kubaini baadhi ya wasanii katika kumbi hizo ni raia wan chi za nje.
Washima
amesema wiki iliyopita idara yake imewakamata wasanii watatu wa bendi ya Super
star ya jijini Mwanza wakiwa Raia wa Nchi ya Kongo ambao walikuwa wakifanya
kazi za muziki bila kibali.
Aidha
Washima amesema kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu na watu hao tayari
wamehukumiwa mahakamani vifungo vya miezi kumi na nne kila mmoja,na kulipa
faini ya Shilingi Laki Moja kwa kila mmoja.
Amesema
kufuatia hali hiyo wamiliki wa kumbi za starehe wanapaswa kufuata sheria kuliko
kuajiri wasanii kutoka nchi za nje bila kibali hali ambayo hata wamiliki
wenyewe idara yake itawachukulia hatua za kisheria.
Amewataja
wasanii waliokamatwa na idara yake na kisha kufungwa jela ni pamoja na Mpiga
gitaa wa bendi wa Super Star,Kashindye Byamungu{18},Dhahiri
Kwamlima{22}mwimbaji pamoja na Edward Wamwamba{25}Mwimbaji wote raia wa nchi ya
Kongo.
إرسال تعليق