HUKU
kukiwa na tabia kuwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito wanakuwa
na tabia za kusumbua na kubagua baadhi ya vitu, msanii wa filamu za
Kibongo Aunty Ezekiel ‘Mama Kijacho’, amesema kwa upande wake yuko vile
vile na wala hajabadilika.
Msanii wa filamu za Kibongo Aunty Ezekiel ‘Mama Kijacho’.
Akimwaga ‘ubuyu’ na Uwazi, Aunty alisema kuwa haoni kama amebadilika
kitabia au kuwa msumbufu bali anajiona yupo kawaida ingawa mara nyingine
anakuwa anachoka sana.
“Mimba wala haijanibadili maisha kwa maana sipo kama wanawake wengine
wanavyokuwa wasumbufu, naamini kuwa nitaendelea kuwa hivi hadi mwisho
nitakapojifungua,” alisema Aunty.

إرسال تعليق