Baraza
la Maadili ya Viongozi wa Umma litawaweka kiti moto watuhumiwa 9 ambao
ni viongozi wanaohusishwa na kashfa ya akaunti ya uchotaji wa fedha
kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Katika
kikao hicho pia viongozi wengine wawili ambao ni Mkuu wa Wilaya ya
Korogwe Mrisho Gambo ambaye ataendelea kubanwa na tume hiyo kwa madai
ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na Meya wa Manispaa ya Tabora
Gullam Hussein Dewji ataendelea kubanwa juu ya ufujaji wa fedha za
manispaa anaodaiwa kuufanya
Viongozi
hao watawekwa kiti moto kwa uwazi mwanzoni mwa mwezi ujao kwenye ukumbi
wa Karimjee, Dar es Salaam. Habari zinaeleza kuwa watakaoitwa ni wale
viongozi wote ambao wanaowajibika chini ya Sheria ya maadili ya viongozi
wa umma.
Taarifa
zilizopatikana kutoka ndani ya tume ya maadili zilieleza kuwa kwa sasa
hati za kuitwa kwa watuhumiwa hao zinaandaliwa, lakini hata hivyo tume
hiyo haikutoa majina ya watuhumiwa hao.
Hata
hivyo sheria ya maadili ya viongozi wa umma inawabana viongozi na
watumishi wa ngazi ya juu wa umma wakiwemo wabunge, majaji, wakuu wa
wilaya, mikoa, majaji na mawaziri, mwanasheria mkuu.
Licha
ya majina ya watuhumiwa hao kutopatikana, lakini chini ya sheria hiyo
viongozi wanaowajibika kwa tume hiyo wako 27 na miongoni mwao wamo
wabunge, wakuu wa wilaya, majaji na hakimu na katibu mkuu wa wizara.
Kwa
hali hiyo wabunge ambao wanatarajia kusimama mbele ya tume hiyo ni wale
ambao walipokea fedha kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering
James Rugemarila ili waeleze mazingira ya kupewa fedha hizo.
Wabunge
hao ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge aliyepokea Sh bilioni
1.6, Mbunge wa Sengerema William Ngeleja ( Sh milioni 40), Mbunge wa
Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka ambaye alipokea Sh bilioni 1.6 na
akajitetea kuwa fedha hizo zilikuwa ni za mchango wa kulipa mkopo wa
shule anayoisimamia.
Pia
Profesa Sospeter Muhongo ambaye amejiuzulu uwaziri wa nishati na madini
hivi karibuni; lakini anabakia na ubunge wake pia anaweza kuitwa mbele
ya tume hiyo aeleze mazingira ya kuruhusu fedha zilizokuwemo kwenye
akaunti ya Tegeta Escrow zichotwe kirahisi.
Wengine
ni majaji Frederick Werema ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wa Serikali
naye ataeleza sababu za kuamuru fedha hizo za Escrow zichotwe. anabanwwa
na kipengele kinachoeleza kuwa anatakiwa kutoa maamuzi kwa mujibu wa
sheria za nchi.
Jaji
Werema katika sakata hilo anatuhumiwa kuvunja sheria za nchi kwa
kuruhusu fedha hizo zichotwe bila kutozwa kodi jambo ambalo Mamlaka ya
Mapato imedai kulikuwa na kodi ya Serikali.
Majaji
wengine ni Dk John Ruhangisa na Aloycsius Mujulizi. Dk Ruhangisa na
Mujulizi wao wamekiri kupokea fedha kutoka kwa Rugemarila. Dk Ruhangisa
alipokea Sh Sh404.25 milioni na Jaji Aloysius K Mujulizi (Sh40.4
milioni).
Pia
yumoa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip
Saliboko (Sh40.4 milioni) ambaye anabanwa na sheria hiyo pia anaweza
kuitwa na tume hiyo.
Wabunge
na majajji ambao wamekiri kupokea fedha hizo wanabanwa na kipengele
kinachoeleza zawadi na fadhila kw aviongozi wa umma kuwa wanatakiwa
wasiombe wala kupokea fadhila za kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo
ukarimu wa kawaida au fadhila nyingine za zawadi za kawaida.
Pia
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi naye anaweza
kuitwa kwenye tume hiyo kwa kuwa bado ni mtumishi wa serikali ambaye
anaendelea kuchunguzwa. Naye anabanwa na kipengele cha utoaji wa maamuzi
aliyoyafanya akiwa madarakani.
Kamishna
wa Tume ya Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda licha ya kukiri kuwepo
kwa suala hilo lakini hakutaka kutoa ufafanuzi wa kina, lakini taarifa
kutoka ndani ya ofisi ya tume ya maadili zinasisitiza kuwa kikao hicho
kitafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao .

إرسال تعليق