Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA imetakiwa
kufanya upya ukokotoaji na kupunguza bei ya mafuta ili mwananchi wa
kawaida anufaike na punguzo la bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia
badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa wa bidhaa hiyo pekee
sambamba na kuangalia namna ya kuishirika sekta binafsi katika sekta ya
gesi.
Agizo hilo la Bunge kupitia kwa kamati ya kudumu ya nishati na
madini limetolewa bungeni mjini Dodoma na Mh .Juma Abdala Jjwayo wakati
akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni ili kuwapa fursa wananchi
kunufaika na punguzo hilo badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa
pekee huku kamati ya kudumu ya bunge ya miundo mbinu Peter Serukamba
akisisitiza ulaazima wa usafiri wa reli kufufuliwa.
Mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo baadhi ya wabunge
waliopata fursa ya kuchangia wametaka serikali kutilia msisitizo kwenye
miundo mbinu inayowagusa watanzania wote badala ya wale wenye kipato cha
juu pekee,pia kupunguzwa kwa bei ya mafuta na nishati pamoja na
kuhakikisha wafanyakazi wanaohudumia sekta ya reli wanalipwa stahiki zao
kwa wakati.
Aidha pia wabunge wengi akiwemo mbunge wa simanjiro Mh. Christopher
Ole Sendeka wamegusia suala la mradi wa usambazaji wa nishati ya umeme
vijijini yaani REA na kutaka serikali kuhakikisha inatenga fedha za
kutosha kuukamilisha mradi huo na kwamba suala la kupeleka na kusimika
nguzo pekee halitoshi.
- ITV
إرسال تعليق