Hili Ndio Tamko la Serikali kuhusu kuitafuta ndege ya AirAsia

Serikali ya Malaysia imesitisha shughuli ya kuitafuta ndege iliyopotea ya MH370 na kusema wanachukulia kama ajali ambayo iliangamiza watu wote.
Tangu kuanza kutafutwa kwa ndege hiyo iliyopotea tangu Machi 8 mwaka jana wakati ikitokea Malaysia kuelekea China hakukuwahi kuwa na dalili yoyote ya kupatikana kwa watu hao wala ndege hiyo.
Maafisa wakuu wanasema shughuli ya kuipata ndege hiyo, bado inaendelea lakini inasemekana abiria 239 waliokuwa kwenye ndege hiyo wote walifariki.
Mmoja wa ndugu wa marehemu waliopotea kwenye ndege hiyo akilia kwa uchungu
Hata hivyo Maofisa wa Serikali wa nchini hiyo walitoa taarifa leo na kusema ndugu na jamaa wa waathirika wa ndege hiyo watalipwa fidia.
Kulingana na picha za Satelite, mabaki ya ndege hiyo huenda yako katika mji wa Perth Magharibi mwa Australia.

Post a Comment

أحدث أقدم