Mpanda. Kijana mmoja aitwaye Michael Edward
(25) mkazi wa Mtaa wa Mji wa Zamani, Mkoa wa Katavi amehukumiwa kifungo
cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumlawiti
mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba.
Hukumu hiyo iliyovuta hisia za watu wengi mjini
Mpanda, ilitolewa juzi na Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo wa pande zote mbili.
Awali, akisoma maelezo ya upande wa mashtaka
Mwendesha Mashtaka, Kulwa Sikwesa alidai mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa
alitenda kosa hilo Oktoba 9, 2014, saa 12 jioni katika eneo la Mji wa
Zamani
Alisema siku hiyo ya tukio mshtakiwa alikutana na
mtoto huyo njiani akielekea nyumbani kwao ndipo alipomshika mkono na
kwenda naye kwenye pagala la nyumba katika mtaa huo.
Mwendesha mashtaka huyo aliieleza Mahakama hiyo
kuwa, baada ya kuingia naye ndani mshtakiwa alitoa kisu na kuchoma
kwenye ubao aliokuwa amemshikisha mtoto huyo ikiwa ni ishara ya
kumtishia kisha alimwambia endapo atakataa kulawitiwa au akipiga kelele
atamuua.
Sikwesa alidai baada ya vitisho hivyo ndipo
mshtakiwa alipomvua nguo mtoto huyo na yeye suruali na kutoa sehemu zake
za siri na kuupaka mate na kisha kuanza kumlawiti mtoto huyo kwa nguvu.
Alidai baada ya kumlawiti alimtishia kutotoa siri hiyo lakini mtoto
huyo baada ya kufika kwa wazazi wake alilazimika kuwaambia kutokana na
maumivu aliyokuwa nayo na ndipo walipotoa taarifa Polisi kabla ya
kukamatwa
Post a Comment