Arusha. Serikali imeahidi kuangalia utaratibu
wa kuanzisha mfumo wa kugharimia elimu ya ufundi nchini ili kuwawezesha
wanafunzi kupata mikopo kama wa elimu ya juu. Lengo likiwa ni kuwapata
wataalamu wa kutosha katika viwanda na sekta nyingine.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Jenista Mhagama alitoa kauli hiyo juzi wakati wa kuwatunuku vyeti
wahitimu wa ngazi mbalimbali katika mahafali ya Sita ya Chuo cha Ufundi
Arusha (ATC). Alisema Serikali inatambua jitihada zinazofanywa na chuo
hicho za kupanua udahili ili kuziba pengo la uhaba wa mafundi sanifu
uliopo nchini.
Katika mahafali hayo, wahitimu wa kwanza katika
fani ya uhandisi wa umeme na vifaatiba walitunukiwa stashahada zao.
Naibu Waziri huyo alisema wataalamu hao watasaidia kutengeneza vifaatiba
katika hospitali jambo litakaloongeza ubora wa huduma za afya na ajira.
Mkuu wa Chuo hicho, Dk Richard Masika aliomba
kuendelea kutolewa kwa Sh10 milioni kwa wanafunzi bora 10 katika masomo
yao. ya mwisho ili kuongeza ushindani katika masomo ya sayansi na ufundi
hapa nchini.
Post a Comment